Mahudhurio ya wanafunzi wa dini katika hafla hizi yalikuwa fursa ya upyaishaji (uhuishaji) wa ahadi kwa misingi ya Muqawama, kutukuza kumbukumbu ya Mashahidi, na kusisitiza juu ya kuendeleza njia ya haki na uadilifu ambayo Sayyid Hassan Nasrallah aliuliwa Kishahidi na kupoteza uhai wake katika kuilinda njia hiyo.

28 Septemba 2025 - 15:22

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa heshima ya kumbukumbu ya shahada ya kiongozi mkubwa wa Muqawama wa Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrallah, kituo cha Kiislamu cha Al-Hadi nchini Malawi kiliandaa mfululizo wa programu za kitamaduni, kidini na kijamii.

Shughuli hizo zilijumuisha mihadhara ya kielimu na kidini, usomaji wa Qur’ani Tukufu, majlisi za maombolezo, pamoja na maonyesho ya filamu na makala zilizobainisha maisha na jihadi za marehemu, pamoja na nafasi yake katika mapambano na mshikamano wa Kiislamu.

Mahudhurio ya wanafunzi wa dini katika hafla hizi yalikuwa fursa ya upyaishaji (uhuishaji) wa ahadi kwa misingi ya Muqawama, kutukuza kumbukumbu ya Mashahidi, na kusisitiza juu ya kuendeleza njia ya haki na uadilifu ambayo Sayyid Hassan Nasrallah aliuliwa Kishahidi na kupoteza uhai wake katika kuilinda njia hiyo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha